Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2017

WAJUMBE WAKIFURAHIA "SELFIE" BAADA YA USAILI WA KARANI WA KIEF TAREHE 23-08-2017

Picha
Wajumbe wa KIEF, Astahili Akilimali, Husna Sungura na Ahmadi Sovu wakijiburudisha na "Selfie" baada ya kazi ya Usaili wa Karani wa KIEF uliofanyika Nur Islamic Magomeni Dar es Salaam.

USAILI WA KARANI WA KIEF ULIOENDESHWA NA JOPO LA USAILI LA KIEF TAREHE 23-08-2017

Picha
Wajumbe wa KIEF, wakiendelea na Usaili wa Karani wa KIEF atakaehudumia ofisi ya KIEF iliyopo Ujiji Kigoma, mtaa wa Lumumba/Buhoro. Mradi wa Masomo ya ziada wa KIEF ukiwa hatua za mwisho kabla ya kuanza.

FURSA YA UDHAMINI WA ASTASHAHADA YA UUGUZI NA UKUNGA KWA WASICHANA MKOA WA KIGOMA KUTOKA BMB-RTz

Picha
Tangazo la Fursa Udhamini wa Elimu kwa Wasichana wa Mkoa wa Kigoma , Elimu ya Ukunga na Uuguzi ngazi ya Astashahada. Ufadhili unaratibiwa na More and Better Midwives For Rural Tanzania. Angalia kipeperushi kwa maelezo zaidi. Mwisho wa Maombi ni Tarehe 30-08-2017

SEHEMU YA VITABU VYA KIADA VILIVYOKUSANYWA WAKATI WA KIKAO

Picha
Hivi ni sehemu ya Vitabu vya kiada vilivyokusanywa kwenye kikao cha Tarehe 13-08-2017 kilichofanyika Nur Islamic Magomeni

UPOKEAJI WA MICHANGO MBALI MBALI ILIYOTOLEWA NA WAJUMBE WA KIEF SIKU YA KIKAO TAREHE 13-08-2017

Picha
Upokeaji wa Michango mbali mbali iliyotolewa na wajumbe wa KIEF siku ya kikao tarehe 13-08-2017 pale Nur Islamic. Mradi huu hutegemea michango ya wanachama wa KIEF kwa ajili ya utekelezaji. Hapa wakikabidhi michango ya Pesa kwa ajili ya ununuzi wa thamani za Ofisi ya KIEF iliyopo Ujiji Kigoma, mtaa wa Lumumba/Buhoro.

WAJUMBE WAKIBADILISHANA MAWAZO NA SHEIKH MUHAMMED SAIDI TAREHE 13-08-2017

Picha
Wajumbe wa KIEF wakibadilishana mawazo na Mwandishi wa Vitabu na Makala Sheikh Mohammed Said wakati wa Kikao cha KIEF kilichofanyika Tarehe 13-08-2017

WAJUMBE WA KIEF NA MWANDISHI NGULI SHEIKH MOHAMMED SAIDI KATIKA PICHA YA PAMOJA KABLA YA KIKAO CHA TAREHE 13-08-2017

Picha
Wajumbe wa KIEF wakiwa katika picha ya pamoja na mwandishi nguli wa vitabu na makala Sheikh Muhammed Saidi kabla ya Kikao cha KIEF kilichofanyika tarehe 13-08-2017 katika shule ya Nur Islamic iliyopo Magomeni.

MAPOKEZI YA VITABU VILIVYOTOLEWA KWA AJILI YA MRADI WA MASOMO YA ZIADA KATIKA KIKAO TAREHE 13-08-2017

Picha
Wajumbe wakipokea na kukagua vitabu vilivyotolewa na wadau kwa ajili ya mradi wa masomo ya ziada kwa wanafunzi wa Shule za Upili za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Unaotarajiwa kuanza hivi karibu. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa kikao cha Wiki cha KIEF kilichofanyika katika shule ya Nur Islamic magomeni.

UDAHILI WA WALIMU WATAKAOSHIRIKI KWA KUJITOLEA KWENYE MRADI WA KIEF 12-08-2017

Picha
Wajumbe wa Kigoma Elimu Foundation, wakiendelea na udahili wa Walimu watakaoshiriki mradi wa KIEF wa masomo ya ziada, unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni katika Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa wanafunzi wa Manispaa hiyo.

WAJUMBE WAKIKAGUA MEZA ILOYOTOLEWA NA MMOJA WA WANA KIEF KWA AJILI YA MRADI 30/07/2017

Picha
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi "Mwalimu wa Kiswahili"Ahmadi Sovu akipokea meza itakayotumika kwenye mradi ofisi ya KIEF Ujiji kutoka kwa mjumbe wa KIEF Mwalimu Astahili Akilimali siku ya tarehe 30-07-2017 baada ya kikao cha Kamati ya Maandalizi

WAJUMBE WA KAMATI WAKIZIKAGUA FULANA HUSIKA 30-07/2017

Picha
Wajumbe wakizikagua fulana zitakazotumiwa na wanafunzi watakaoshiriki Mradi wa Masomo ya Ziada utakaoendeshwa na KIEF kwa wanafunzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji

FULANA ZA MFANO ZITAZOTUMIWA NA WANAFUNZI WANAOSHIRIKI MRADI ZIKIKABIDHIWA KWA KAMATI TAREHE 30/07/2017

Picha
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi akikabidhi Fulana za mfano zitakazotumiwa na wanafunzi watakaoshiriki mradi wa Masomo ya Ziada utakaoendeshwa na KIEF manispaa ya Kigoma Ujiji. Fulana hizi ni sehemu ya mpango wa kuutangaza mradi kwa Jamii.

WAJUMBE WA KAMATI YA KIEF KATIKA KIKAO CHA TAREHE 30/07/2017 DAR ES SALAAM

Picha
Wajumbe wakiendelea na mjadala katika kikao cha maandalizi ya mradi wa masomo ya ziada kwa wanafunzi wa Sekondari wa Manispaa ya Kigoma Ujiji unaotarajiwa kuanza hivi karibu