Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Nuur Islamic

SURA ZA TABASAMU ZA WANA KIEF KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA KIKAO CHA TAREHE 24-09-2017

Picha
Picha ya pamoja ya wana KIEF baada ya kikao cha maandalizi ya mpango wa mafunzo ya ziada kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari Manispaa ya Kigoma Ujiji, unaotarajiwa kuanza mwezi wa Kumi, ukihusisha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu 2017.

WAJUMBE WAKIENDELEA NA KIKAO CHA MAANDALIZI LEO TRH 24/9/2017

Picha
Wajumbe wa KIEF wakiendelea na kikao cha maandalizi ya program ya masosmo ya ziada inayotarajiwa kuanza mwezi wa Kumi katika kituo cha shule ya msingi Ujiji.

WAKILI MSOMI WA KIEF AKIWASILISHA RASIMU YA KATIBA YA KIEF KWENYE KIKAO CHA TAREHE 27/08/2017

Picha
Wakili Msomi Ibrahim Shineni, akiwasilisha mbele ya wajumbe wa KIEF rasimu ya katiba katika kikao kilichofanyika tarehe 27/08/2017 Jijini Dar es Salaam.

WALIO MBALI HUSHIRIKI VIKAO KWA NJIA YA MTANDAO

Picha
Wajumbe wakimsikiliza kwa makini Mjumbe wa KIEF Bakari Issa alliye masomoni India akiwasilisha maoni yake kuhusu katiba ya KIEF kupitia njia ya mtandao katika kikao cha tarehe 27/08/2017. Njia hii imekuwa ikiwapa fursa walio mbali kushiriki vikao moja kwa moja kwa njia ya mtandao.

WAJUMBE WA KIEF WAKIPATA CHAKULA CHA MCHANA TAREHE 27/08/2017

Picha
Picha mbali mbali wakati wajumbe wa KIEF wakipata chakula cha mchana kabla ya kikao cha Mjadala wa Katiba kilichofanyika Nur Islamic Secondary School Magomeni tarehe 27/08/2017.

USAILI WA KARANI WA KIEF ULIOENDESHWA NA JOPO LA USAILI LA KIEF TAREHE 23-08-2017

Picha
Wajumbe wa KIEF, wakiendelea na Usaili wa Karani wa KIEF atakaehudumia ofisi ya KIEF iliyopo Ujiji Kigoma, mtaa wa Lumumba/Buhoro. Mradi wa Masomo ya ziada wa KIEF ukiwa hatua za mwisho kabla ya kuanza.

SEHEMU YA VITABU VYA KIADA VILIVYOKUSANYWA WAKATI WA KIKAO

Picha
Hivi ni sehemu ya Vitabu vya kiada vilivyokusanywa kwenye kikao cha Tarehe 13-08-2017 kilichofanyika Nur Islamic Magomeni

UPOKEAJI WA MICHANGO MBALI MBALI ILIYOTOLEWA NA WAJUMBE WA KIEF SIKU YA KIKAO TAREHE 13-08-2017

Picha
Upokeaji wa Michango mbali mbali iliyotolewa na wajumbe wa KIEF siku ya kikao tarehe 13-08-2017 pale Nur Islamic. Mradi huu hutegemea michango ya wanachama wa KIEF kwa ajili ya utekelezaji. Hapa wakikabidhi michango ya Pesa kwa ajili ya ununuzi wa thamani za Ofisi ya KIEF iliyopo Ujiji Kigoma, mtaa wa Lumumba/Buhoro.

WAJUMBE WA KIEF NA MWANDISHI NGULI SHEIKH MOHAMMED SAIDI KATIKA PICHA YA PAMOJA KABLA YA KIKAO CHA TAREHE 13-08-2017

Picha
Wajumbe wa KIEF wakiwa katika picha ya pamoja na mwandishi nguli wa vitabu na makala Sheikh Muhammed Saidi kabla ya Kikao cha KIEF kilichofanyika tarehe 13-08-2017 katika shule ya Nur Islamic iliyopo Magomeni.

MAPOKEZI YA VITABU VILIVYOTOLEWA KWA AJILI YA MRADI WA MASOMO YA ZIADA KATIKA KIKAO TAREHE 13-08-2017

Picha
Wajumbe wakipokea na kukagua vitabu vilivyotolewa na wadau kwa ajili ya mradi wa masomo ya ziada kwa wanafunzi wa Shule za Upili za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Unaotarajiwa kuanza hivi karibu. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa kikao cha Wiki cha KIEF kilichofanyika katika shule ya Nur Islamic magomeni.
Picha
IFTAR SESSION FOR KIEF MEMBERS 12-06-2017 AT NUUR ISLAMIC SECONDARY SCHOOL: Members of the KIEF in the picture getting Iftar during Ramadan, after finishing meeting session for the Foundation.