Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Masomo

KIKAO CHA KIEF TAREHE 3 DESEMBA 2017 NUR ISLAMIC MAGOMENI

Picha
Wajumbe wa KIEF wakiwa kwenye kikao cha kawaida kwa ajili ya kupanga shughuli mbali mbali za KIEF. Kikao kilifanyika tarehe 3/12/2017 kwa ajili ya maandalizi ya uzinduzi wa Mradi wa Masomo ya Ziada kwa shule za sekondari ambao umeanza tangu 16/10/2017 katika eneo la Mradi shule ya Msingi Ujiji

TAARIFA YA KUANZA KWA MRADI WA MASOMO WA KIEF TAREHE 16-10-2017

Picha
Wanafunzi wote waliochukua fomu na kuzirejesha za kujiunga na masomo ya ziada ktk Mradi unaodhaminiwa na Asasi ya KIEF mnaarifiwa kuwa masomo yataanza rasmi J umatatu Tarehe 16/10/2017 Saa 10 Jioni Shule ya Msingi Ujiji. Wanafunzi na wazazi/walezi wa wanafunzi hao mmetumiwa ujumbe kwenye Namba za simu mlizojaza kwenye fomu. Ujumbe huo umewajulisha juu ya kuchaguliwa kwenu kujiunga na program hii maalumu. KIEF inawapongeza wote walichaguliwa na pindi nafasi zikiongezeka, wale walioomba awamu hii watahudumiwa kwanza.

MHANDISI MBAROUK MAKUKA KATIKA HARAKATI ZA KULIPIA ANKARA YA TANESCO KWA AJILI YA UJIJI PRIMARY LEO TRH 12-10-2017

Picha
Picha mbalimbali zikimuonyesha Mhandisi Mbarouk Makuka wakati wa harakati ya kulipia gharama za kuunganisha umeme kwenye shule ya Msingi Ujiji iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji. Msaada wa kiasi cha Shilingi za Kitanzania 320,000 zimetolewa na wadau wa KIEF kupitia mwana KIEF Husna Sungura kwa ajili ya kugharamia mchakato huo. KIEF inatanguliza shukurani kwa Wadau wanaotuunga mkono.

MAKABIDHIANO YA MALIPO YA KUUNGANISHA UMEME SHULE YA MSINGI UJIJI LEO TRH 12-10-2017

Picha
Mapema leo hii  tarehe 12-10-2017 Mhandisi Mbarouk Makuka ,(pichani kulia) Mratibu wa muda wa Asasi ya kielimu ya Kigoma Elimu Foundation (KIEF) yenye maskani yake katika viunga vya Manispaa ya Ujiji -Kigoma akimkabidhi  Mkuu wa Shule Ndugu Moses Wilbroad (pichani kushoto) h 320,000/= kwa ajili kuvuta umeme katika majengo ya shule ya msingi Ujiji ati ya malipo ya shilingi za Tanzania Fedha hizo zimetolewa na wana Asasi hiyo ikiwa ni sehemu ya kusaidia kusukuma gurudumu la MAENDELEO ya Taaluma ya mkoa wa Kigoma. Tunakushukuruni kwa kuendelea kujinyima na kusaidia wadogo zetu waweze kufanya vema katika masomo yao.

OFISI IKIWEKWA SAWA TAYARI KWA UTOAJI WA FOMU LEO TRH 2-10-2017

Picha
Wajumbe wa KIEF wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho leo asubuhi kwenye Ofisi za KIEF zilizopo Lumumba/Buhoro mkabala na Uwanja wa Kawawa Ujiji.

HARAKATI ZA KUBANDIKA MATANGAZO MITAA YA UJIJI LEO TRH 2-10-2017

Picha
Mjumbe wa KIEF, Mwalimu Mbaruku Makuka akibandika matangazo yanayohusu mpango wa KIEF wa masomo ya ziada kwa wanafunzi wa sekondari unaotarajiwa kuanza hivi karibuni kwenye mitaa mbali mbali ya Ujiji. Uchukuaji wa fomu za maombi umeanza leo kwenye ofisi ya KIEF iliyopo Kona ya Lumumba na Mtaa wa Buhoro Ujiji, Mkabala na uwanja wa Kawawa.

SURA ZA TABASAMU ZA WANA KIEF KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA KIKAO CHA TAREHE 24-09-2017

Picha
Picha ya pamoja ya wana KIEF baada ya kikao cha maandalizi ya mpango wa mafunzo ya ziada kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari Manispaa ya Kigoma Ujiji, unaotarajiwa kuanza mwezi wa Kumi, ukihusisha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu 2017.

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO YA ZIADA KWA UDHAMINI WA KIEF

Picha
TANGAZO LA MASOMO YA ZIADA  CHINI YA UDHAMINI WA KIGOMA ELIMU FOUNDATION (KIEF)