Machapisho

HARAKATI ZA KUBANDIKA MATANGAZO MITAA YA UJIJI LEO TRH 2-10-2017

Picha
Mjumbe wa KIEF, Mwalimu Mbaruku Makuka akibandika matangazo yanayohusu mpango wa KIEF wa masomo ya ziada kwa wanafunzi wa sekondari unaotarajiwa kuanza hivi karibuni kwenye mitaa mbali mbali ya Ujiji. Uchukuaji wa fomu za maombi umeanza leo kwenye ofisi ya KIEF iliyopo Kona ya Lumumba na Mtaa wa Buhoro Ujiji, Mkabala na uwanja wa Kawawa.

SURA ZA TABASAMU ZA WANA KIEF KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA KIKAO CHA TAREHE 24-09-2017

Picha
Picha ya pamoja ya wana KIEF baada ya kikao cha maandalizi ya mpango wa mafunzo ya ziada kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari Manispaa ya Kigoma Ujiji, unaotarajiwa kuanza mwezi wa Kumi, ukihusisha wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha tatu 2017.

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO YA ZIADA KWA UDHAMINI WA KIEF

Picha
TANGAZO LA MASOMO YA ZIADA  CHINI YA UDHAMINI WA KIGOMA ELIMU FOUNDATION (KIEF)

WAJUMBE WAKIENDELEA NA KIKAO CHA MAANDALIZI LEO TRH 24/9/2017

Picha
Wajumbe wa KIEF wakiendelea na kikao cha maandalizi ya program ya masosmo ya ziada inayotarajiwa kuanza mwezi wa Kumi katika kituo cha shule ya msingi Ujiji.

WAKILI MSOMI WA KIEF AKIWASILISHA RASIMU YA KATIBA YA KIEF KWENYE KIKAO CHA TAREHE 27/08/2017

Picha
Wakili Msomi Ibrahim Shineni, akiwasilisha mbele ya wajumbe wa KIEF rasimu ya katiba katika kikao kilichofanyika tarehe 27/08/2017 Jijini Dar es Salaam.

WALIO MBALI HUSHIRIKI VIKAO KWA NJIA YA MTANDAO

Picha
Wajumbe wakimsikiliza kwa makini Mjumbe wa KIEF Bakari Issa alliye masomoni India akiwasilisha maoni yake kuhusu katiba ya KIEF kupitia njia ya mtandao katika kikao cha tarehe 27/08/2017. Njia hii imekuwa ikiwapa fursa walio mbali kushiriki vikao moja kwa moja kwa njia ya mtandao.

WAKATI WA KUBADILISHANA MAWAZO KABLA YA KIKAO CHA TAREHE 27/08/2017

Picha
Wajumbe wa KIEF wakibadilishana mawazo kabla ya kikao cha kujadili katiba cha tarehe 27/08/2017