Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2017

TAARIFA YA TUME YA VYUO VIKUU KUHUSU WANAFUNZI WALIOPATA NAFASI ZAIDI YA MOJA YA CHUO

Picha
Kuona majina ya mabao hawajathibitisha  || Kuona majina ya waliothibitisha zaidi ya chuo kimoja  || Kuona majina ya Waliothibitisha Vyuoni na Kuomba tena vyuo vingine

TAARIFA YA KUANZA KWA MRADI WA MASOMO WA KIEF TAREHE 16-10-2017

Picha
Wanafunzi wote waliochukua fomu na kuzirejesha za kujiunga na masomo ya ziada ktk Mradi unaodhaminiwa na Asasi ya KIEF mnaarifiwa kuwa masomo yataanza rasmi J umatatu Tarehe 16/10/2017 Saa 10 Jioni Shule ya Msingi Ujiji. Wanafunzi na wazazi/walezi wa wanafunzi hao mmetumiwa ujumbe kwenye Namba za simu mlizojaza kwenye fomu. Ujumbe huo umewajulisha juu ya kuchaguliwa kwenu kujiunga na program hii maalumu. KIEF inawapongeza wote walichaguliwa na pindi nafasi zikiongezeka, wale walioomba awamu hii watahudumiwa kwanza.

MHANDISI MBAROUK MAKUKA KATIKA HARAKATI ZA KULIPIA ANKARA YA TANESCO KWA AJILI YA UJIJI PRIMARY LEO TRH 12-10-2017

Picha
Picha mbalimbali zikimuonyesha Mhandisi Mbarouk Makuka wakati wa harakati ya kulipia gharama za kuunganisha umeme kwenye shule ya Msingi Ujiji iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji. Msaada wa kiasi cha Shilingi za Kitanzania 320,000 zimetolewa na wadau wa KIEF kupitia mwana KIEF Husna Sungura kwa ajili ya kugharamia mchakato huo. KIEF inatanguliza shukurani kwa Wadau wanaotuunga mkono.

MAKABIDHIANO YA MALIPO YA KUUNGANISHA UMEME SHULE YA MSINGI UJIJI LEO TRH 12-10-2017

Picha
Mapema leo hii  tarehe 12-10-2017 Mhandisi Mbarouk Makuka ,(pichani kulia) Mratibu wa muda wa Asasi ya kielimu ya Kigoma Elimu Foundation (KIEF) yenye maskani yake katika viunga vya Manispaa ya Ujiji -Kigoma akimkabidhi  Mkuu wa Shule Ndugu Moses Wilbroad (pichani kushoto) h 320,000/= kwa ajili kuvuta umeme katika majengo ya shule ya msingi Ujiji ati ya malipo ya shilingi za Tanzania Fedha hizo zimetolewa na wana Asasi hiyo ikiwa ni sehemu ya kusaidia kusukuma gurudumu la MAENDELEO ya Taaluma ya mkoa wa Kigoma. Tunakushukuruni kwa kuendelea kujinyima na kusaidia wadogo zetu waweze kufanya vema katika masomo yao.

OFISI IKIWEKWA SAWA TAYARI KWA UTOAJI WA FOMU LEO TRH 2-10-2017

Picha
Wajumbe wa KIEF wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho leo asubuhi kwenye Ofisi za KIEF zilizopo Lumumba/Buhoro mkabala na Uwanja wa Kawawa Ujiji.

TANGAZO LILILOBANDIKWA KWENYE MAENEO YA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI

Picha
Tangazo likiwa limebandikwa kwenye 'mrangi' kwa ajili ya kuwatangazia wakazi wa Kigoma Ujiji fursa ya Masomo ya ziada wa wanafunzi wa sekondari inayoendeshwa na KIEF leo tarehe 2-10-2017

HARAKATI ZA KUBANDIKA MATANGAZO MITAA YA UJIJI LEO TRH 2-10-2017

Picha
Mjumbe wa KIEF, Mwalimu Mbaruku Makuka akibandika matangazo yanayohusu mpango wa KIEF wa masomo ya ziada kwa wanafunzi wa sekondari unaotarajiwa kuanza hivi karibuni kwenye mitaa mbali mbali ya Ujiji. Uchukuaji wa fomu za maombi umeanza leo kwenye ofisi ya KIEF iliyopo Kona ya Lumumba na Mtaa wa Buhoro Ujiji, Mkabala na uwanja wa Kawawa.